Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amehoji iwapo ni sahihi kwa Kanuni za Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019 kuanza kutumika kabla ya Kamati ya Sheria ndogo kuzipitia.

Amehoji swali hilo mara baada ya kupata nafasi kuuliza swali la nyongeza katika kipindi cha maswali na majibu bungeni jijini Dodoma.

Amesema kuwa inawezekana watu wakaona mambo ya Uchaguzi huo wa serikali za mitaa ni madogo lakini amani ya nchi inaweza kupotea ama kuathirika kama mambo hayo yasipopewa kipaumbele.

Aidha, amesema kuwa sheria ndogo na kanuni zinazotungwa zozote lazima ziangaliwe bungeni lakini vikao vinavyokaa kujadili mabadiliko ya sheria haviwezi kuwa mbadala wa Bunge.

”Mheshimiwa Waziri atueleze katika utamaduni huo ambako kanuni tayari zimeshaingizwa kazini, huku kamati ndogo haikuzipitia kwa kisingizio cha kwamba wadau walizipitia, jambo ambalo siyo kweli,”amesema Mbowe

Hata hivyo, ameongeza kuwa kamati ndogo ya bunge haijawahi kupitia wala kuziona kanuni za uchaguzi wa serikali za mitaa.

TFF yawashukuru wadau wa Soka nchini
Waziri Kigwangalla aonya, 'Natoa huruma ya mwezi mmoja tu'