Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amewataka watu wanaosimamia usalama wa nchi wawe makini kwa kile wanachokilinda lasivyo watajikuta wanaiteketeza nchi bila ya wao wenyewe kujijua

Ameyasema hayo mapema hii leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa kauli za viongozi wa ngazi za juu ni za msingi pale zinapotolewa kulinagana na katibana sheria zinavyosema.

“Taifa lolote huongozwa na katiba pamoja na Sheria zake, na sheria huongozwa na kanuni. tunapokuwa tunapuuza sheria zetu, tunapuuza mikataba yetu, mtawala yeyote anapofikili yupo juu ya sheria, juu ya mikataba, mwisho wa siku wanaoumia ni watanzania. Kwa sababu Jumuiya na Jamii za Kimataifa inatambua sheria za Tanzania na wala haitambui kauli za viongozi wa taifa. Rais apongezwe pale anapofanya jambo jema lakini afanye jambo jema kwa misingi ya Sheria, Katiba na Kanuni ikiwemo na mikataba tuliyojiwekea,”amesema Mbowe

Aidha, Mbowe amewataka wananchi kutokuwa wepesi wa kushangilia jambo linalokuwa linazungumzwa na kiongozi, kwani si jambo jema kuupima na kuchuja kauli za viongozi kabla ya kuwashangilia.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kama Rais anapokuwa amefanya jambo zuri na lenye manufaa kwa jamii basi anastahili kupewa pongezi bila ya uoga wowote kwani anakua ametekeleza majukumu yake.

 

 

IGP Sirro: Kustaafu kazi sio mwisho wa kufanyakazi jeshini
Lema ampigia magoti JPM, amtaka aruhusu maandamano