Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa ameshangazwa na kitendo cha Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kusema kuwa Serikali iko tayari kumtibu Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu popote duniani.

Ameyasema hayo hii leo jijini Dar es salaam alipokuwa akitoa taarifa kuhusu matibabu ya Lissu yanayoendelea jijini Nairobi. ambapo amesema kuwa wakati walipoamua kumpeleka Lissu jijini Nairobi, Waziri Ummy alikuwepo lakini walitaka Lissu apelekwe Muhimbili kwanza na baadaye kama angepata rufaa angepelekwa nchini India.

“Ilikuwa ni hatari na ni maamuzi yalikuwa magumu sana, watu ambao wana mamlaka, Waziri wa Afya yuko pale, Spika yuko pale nawaambia fanyeni maamuzi tumuokoe huyu mtu wanasema hatuwezi kumpeleka Nairobi, mimi nikasisitiza sisi tunampeleka Nairobi wakasema basi utalipa mwenyewe, nikasema sawa tutalipa wenyewe.”amesema Mbowe

Hata hivyo, ameongeza kuwa siku za hivi karibuni alimtafuta Spika wa bunge kupitia wasaidizi wake kumtaarifu kwamba Serikali inaweza kusaidia matibabu ya Lissu lakini kwa masharti matatu, ikiwa ni wakubali apelekwe India, aandikie barua ya maombi na tatu apeleke taarifa yote kuhusu matibabu ya hospital ya mgonjwa na kwa upade wake alikataa.

Dkt. Abbass: Kibiti wazungu hawakuja kuchunguza
Serikali yapewa masaa 72 kuishtaki IEBC