Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (Chadema), Mhe, Freeman Mbowe amesema tendo la madiwani wake 46 kuhamia (CCM) kinawapa funzo katika maandalizi ya kutafuta viongozi ambao ni wa kweli wanaoweza kusimamia chama na si wale wanaotafuta njia ya kutoka kupitia uongozi.

Mbowe amesema Kitendo cha madiwani 46 kuhamia CCM si kukiuwa Chadema kwani nchi nzima Chadema inamadiwani zaidi ya 1130, ameongezea kuwa madiwani hao kujiuzulu ni jambo linalofanywa na CCM kwa lengo la kuwakatisha tamaa wana Chadema.

“Kazi kubwa inayofanywa na CCM ni kuwakatisha tamaa ni jambo ambalo limefanyika karibuni ambalo linaonekana wana CHADEMA wengi wamerudishwa nyuma basi ni suala la madiwani, madiwani wamenunuliwa jamanii wanaunga mkono juhudi, kuna watu wengine ni mizigo lakini sasa tunafanyaje lakini watu wa CHADEMA wanakata tamaa eti madiwani wanaisha chama kinakufa, hiki chama hakifi mzee CHADEMA nchi nzima ina madiwani 1184 madiwani mpaka dakika hii wameondoka ni madiwani 46 kwa hiyo tuna madiwani zaidi ya 1130 wamebaki CHADEMA halafu mtu anasema CHADEMA inakufa una akili wewe?.

Mboye ameongezea kuwa ”Kwetu ni funzo tunapojiandaa kwenda kwenye uchaguzi wa Wenyeviti wa Mtaa, Vijiji, madiwani, wabunge hata nafasi ya Urais tukajiandaa na kina nani wanaoishi ndoto ya CHADEMA lazima safari hii tujiridhishe mapema huyu tukimpa nafasi basi historia yake tunaijua vyema”.

Serikali yakanusha kupiga marufuku mikutano ya kisiasa
Saudi Arabia yaruhusu ujenzi wa makanisa