Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa kitu kikubwa kinachomsumbua ni msongo wa mawazo.

Ameyasema wakati akizungumza na baadhi ya waandishi wa habari waliofika katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es salaam alikokuwa amelazwa.

Amesema kuwa kwasasa afya yake inaendelea vizuri hivyo baada tu ya kumaliza msiba ataendelea kufanya vipimo maalumu vya kiafya kwa kadiri ambavyo atatakiwa na madaktari wake kama itakuwa ndani au nje ya nchi.

Hata hivyo, Mbowe amewashukuru viongozi wa vyama mbalimbali pamoja na Watanzania ambao walimtembelea na hata waliokuwa wakimuombea kwa njia mbalimbali katika kipindi hiki yeye na familia yake ikiwa na wale ambao walizuiwa kumuona kutokana na sheria za kitabibu.

 

TFF kushirikiana na 'La Liga' kuinua soka nchini
CBF walalamika FIFA, wataka VAR itumike ipasavyo