Mwenyekiti Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amesema kuwa katika uchaguzi huu mdogo wa marudio katika majimbo mawili ya Kinondoni na Siha jeshi la polisi liandae magereza ya kutosha kwani watawafunga wote na kudai hawawezi kukubali kura kuibiwa.

Ameyasema hayo kwenye kampeni za CHADEMA Magomeni jijini Dar es salaam ambapo amedai Chama Cha Mapinduzi (CCM) bila polisi ni wepesi na hawawezi chochote sababu chama hicho kimeshapoteza mvuto kwa wananchi.

“Yaani nyinyi polisi muachie CCM dakika tano tu wacheze ngoma siku ya tarehe 17 hawa jamaa ni weupe, na polisi ndugu zangu safari hii mtuandalie magereza mtatufunga wote haki ya Mungu, safari hii haibiwi mtu kura hiyo nawaambia mtatuua. Kama tumeweza kupona risasi 38 sasa tupo tayari kwa lolote, Wabunge wetu wanafungwa, wanafukuzwa Bungeni, madiwani wanalazimishwa kuhama chama, kila siku viongozi wa upinzani ni polisi na mahakamani,”amesema Mbowe

Hata hivyo, Mbowe amesema kuwa endapo watafanyiwa mambo ambayo walifanyiwa kwenye uchaguzi wa Kata 43 basi mambo hayawezi kuwa mazuri.

Diamond ampokea Wema kikuza sauti na ‘I love you die’
Magazeti ya Tanzania leo Januari 30, 2018