Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameSsema kuwa kama Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na serikali haioni umuhimu na uwepo wa vyama vingi nchini watumie uwingi wao bungeni wavifute vyama hivyo.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema kuwa toka imeingia madarakani Serikali ya awamu ya tano watu wa upinzani wanaonekana ni maadui.

“Tumemwambia Rais mara nyingi na chama chake kama wao wanaamini upinzani ni hasara kwa nchi na hawajaweza kuona faidi ya vyama vingi vya siasa, kama Chama Cha Mapinduzi hakijaona umuhimu vyama vingi vya siasa kwenye nchi hii kwa miaka 25 hii wana wingi wa kutosha bungeni ni bora wafute vyama vingi lakini ku pretend tupo kwenye vyama vingi wakati mnavikandamiza na kuvifunga mikono wakati nyinyi mnafanya siasa wenzenu wasifanye siasa,”amesema Mbowe 

Hata hivyo, Mbowe amesema kuwa kupitia chama chake cha CHADEMA kwa mwaka 2018 watakuwa na kazi ya kupigania mchakato wa Katiba Mpya pamoja Tume Huru ya Uchaguzi na kusema hilo wanaliweka wazi mapema ili ifahamike.

Huu ni ukakasi mkubwa- Nape
Weah awataka raia wa Liberia walio nje kurudi kuijenga nchi