Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe amesema  Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Katibu wa Kanda ya Nyasa, Emmanuel Masonga wameachiwa huru ghafla hivyo watashughulikia jambo hilo ili kuhakikisha wanaliweka sawa.

Mbowe amesema kuwa hawana uhakika na utaratibu uliotumika kufupisha kifungo chao kwani bado haijawekwa wazi ni kwanini wametumikia kifungo cha miezi mitatu baada ya miezi mitano kama ambavyo mahakama iliwahukumu hapo awali.

Hata hivyo Mbowe amesema baada ya hukumu ya kifungo cha miezi mitano kutolewa mawakili wa wawili hao waliomba kukata rufaa ya hukumu hiyo katika mazingira ya dharura lakini hawakufanikisha.

Pia Mbowe amesema wataendelea kukata rufaa ya kesi yao hata kama wameachiwa leo ili kuhakikisha wanaweka rekodi sawa kwa usahihi ili wasije kuhukumiwa tena kwa makosa ambayo hayakustahili.

Mbowe ametoa taarifa hiyo kupitia ukurasa wake wa instagram.

Aidha Mbunge Josemph Mbilinyi na Katibu Masonga walitiwa hatiani kwa kosa la kutoa lugha ya kashfa dhidi ya Rais Magufuli pindi wakiendesha mkutano wa hadhara.

 

Trump akutana na waliokuwa wafungwa Korea Kaskazini
Heche akerwa na serikali ya CCM aitaka iwe sikivu