Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Simon Sirro, wanatarajia kuwa mashahidi kwenye kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe na wenzake watatu.

Hayo yameelezwa na kiongozi wa jopo la mawakili upande wa utetezi Peter Kibatala mbele ya Hakimu Mkazi mwandamizi Thomas Simba wakati kesi hiyo inatajwa kwa ajili ya kusomwa hati ya mashtaka na Ushahidi kwa hatua za  awali.

Kibatala ameieleza mahakama ya Hakimu kazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo Jumatatu (Agosti 23-2021) baada ya upande wa mashtaka kumaliza kuwasomea maelezo ya awali, (Mbowe na wenzake Watatu).

Malengo ya Wizara ya Madini kukusanya Bilioni 650
Nyumba za nyasi na udongo kutolipiwa kodi