Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amefiwa na mama mkwe wake, Johara Mtei ambaye alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya Agakani Jijini Dar es Salaam.

Marehemu Johara alikuwa mke wa Edwin Mtei, mwasisi wa CHADEMA ambaye pia amewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kati ya Juni 1966 hadi Januari 1974  katika utawala wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, amefikwa na umauti huo leo Ijumaa Agosti 20.

Mashinda Mtei ambaye ni  Mtoto wa Edwin mtei amesema, ni kweli mama yao amefariki na kwa sasa wanaelekea Mkoani Arusha kutoka Dar es Salaam kwaajili ya maandalizi ya maziko.

Msiba huu umetokea ikiwa ni siku 28 zimepita tangu mbowe alipompoteza baba yake mdogo, Manase Alphayo Mbowe. Manase alifikwa na umauti Julai 23 mwaka huu katika Hospitali ya Machame Mkoani Kilimanjaro alikokuwa anapatiwa matibabu baada ya kusikia taarifa za mwanae mbowe kufunguliwa kesi ya ugaidi.

Mbowe ambaye ni mume wa Dkt Lilian binti wa Edwin Mtei na marehemu Johara amepokea taarifa ya vifo hivyo wakati akiwa mahabusu kwenye Gereza kuu la Ukonga jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za uhujumu uchumi na kupanga njama za ugaidi.

Huu ni msiba wa tatu kumkuta Mbowe ndani ya wiki chache, baada ya kaka yake, Charles Mbowe, kufariki Dunia Julai 8 mwaka huu.

Tanzania yapokea mkopo wa tilioni 2.7
Taliban wafanya msako nyumba kwa nyumba