Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.

Amesema kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.

“Alikuwa hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema Mbowe

Aidha, Masha alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola.

Boti yazama ziwa Victoria ikiwa na watu 17
LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Novemba 16, 2017