Kesi inayowakabili Viongozi Wakuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo na Wabunge 7 wa (CHADEMA), imeendelea ambapo imepangiwa Hakimu mpya anayejulikana kwa jina la Kelvin Mhina.

Hatua hiyo ya kesi hiyo Na.112/2018 kupangiwa Hakimu mpya imekuja mara baada ya aliyekuwa Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Dar es salaam, Wilbard Mashauri kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania baada ya kuteuliwa na Rais Dkt. Magufuli Januari 28.

Wakati akiwa Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri aliwafutia dhamana viongozi wawili wa CHADEMA, M/Kiti , Mbowe na Mbunge Esther Matiko kutokana na kushindwa kutimiza masharti ya dhamana waliyopewa na Mahakama.

Aidha, katika kesi hiyo ya viongozi wa CHADEMA, Hakimu mpya Kelvin Mhina, ameahirisha kesi hiyo hadi Februari 14, 2019 itakapotajwa tena baada ya Wakili wa Serikali, Wankyo Simon kutoa taarifa kwamba kesi hiyo ilienda kwa ajili ya kutajwa na kwamba wanasubiri uamuzi wa mahakama ya rufaa.

Hata hivyo, amesema kuwa upande wa mashtaka ulikata rufaa kupinga dhamana, hivyo kesi hiyo itaanza kusikilizwa Februari 18, 2019, ambapo Mbowe na Matiko bado wanaendelea kusota rumande kutokana na kufutiwa dhamana.

 

 

Malori 8 ya Mbao na Mkaa yakamatwa na TRA Njombe
Majaliwa amuwakilisha JPM katika mazishi ya mke wa Mufti wa Tanzania