Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho akiwepo Katibu Mkuu Dkt Vincent Mashinji, John Mnyika, Salum Mwalimu na Ester Matiko wamewekwa mahabusu mara baada ya kuripoti katika kituo cha polisi.

Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Habari CHADEMA Tumaini Makene amethibitisha hilo na kusema kuwa viongozi hao wamewekwa mahabusu baada ya kuripoti Kituo Kikuu Cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao.

“Viongozi Wakuu wa Chama pamoja na wabunge waliokuwa wameripoti Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam wakitimiza masharti ya dhamana yao, wamewekwa mahabusu. Polisi hawajaeleza sababu ya kufanya hivyo. Mawakili wetu wanashughulikia. Tutaendelea kuwapatia taarifa zaidi” amesema Makene.

Aidha Makene amesema kuwa viongozi hao wamefutiwa dhamana yao kwa maelekezo ya Mkuu wa Upelelezi Makosa ya Jinai Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO) pia jeshi la polisi limedai viongozi hao watafikishwa mahakamani Jumatano, Machi 28, mwaka huu.

Kesi hiyo ni kufuatia fujo za maandamano zilizotokea kipindi cha uchaguzi wa diwani kinondoni na kupelekea kifo cha mwanafunzi wa NIT, Akwilina Akwiline baada ya kupigwa risasi na mmoja wa askari katika haraki za kutuliza ghasia ya maandamano hayo ambayo yalikuwa yakipinga zoezi zima la upigaji kura lililodaiwa kutendeka bila kuzingatia haki.

Njombe Mji FC warejea TFF, Bodi ya ligi
Bodi ya ligi yapangua mchezo mwingine