Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe aamesema kuwa amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kifo cha Mkuu wa Idara ya sanaa wa chama hicho, Fullgency Mapunda (Mwana Cotide) aliyefariki dunia Oktoba 6, 2019 saa kumi na dakika ishirini usiku baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Marehemu Fullgency Mapunda alifariki akiwa katika Hospitali ya St. Monica iliyopo Manzese Jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Enzi za uhai wake aliimba wimbo wa chama hicho wenye maneno “CHADEMA People’s Power” ambao ni maarufu.

Kupitia ukurasa wa instagram wa Freeman Mboye ametuma salamu za pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na kijana wao ambayo bado umri wake bado mdogo kuaga dunia.

”Nimepokea kwa huzuni kubwa kifo cha Kamanda wetu, ni mapema sana kamanda (Fullgence Mapunda also known as Mwanacotide) umeondoka, tutakukumbuka kwa mazuri yako, kimwili haupo nasi lakini utaishi kwenye mioyo ya walio wengi kupitia muziki wako, ulitunga nyimbo nzuri za hamasa katika chama chetiu cha Chadema, pamoja na zile za kupigania haki katika taifa letu, ambazo zitafanya tukukumbuke kila zitakaosikika masikioni mwetu,” Mbowe ambaye ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ameandika.

“Mara ya mwisho nilikutembelea hospitalini tuliongea mambo mengi, ulisema umefurahi sana kuniona, nikakwambia ni kawaida mtu anapougua kumjulia hali na kufarijiana…” ameongeza.

 

Wanafunzi 8 mbaroni kwa kumsababishia mwenzao kifo
Waziri Mkuu amsweka ndani afisa aliyenunua vifaa vya ujenzi kwenye duka la nguo