Kimbunga cha msako wa watumishi hewa kina kila dalili ya kuwasomba wadogo na vigogo, baada ya Mbunge wa Makete (CCM), Profesa Norman Sigalla kudaiwa kutafuna mishahara mitano ya ukuu wa wilaya asiyoifanyia kazi.

Imedaiwa kuwa Profesa Sigalla aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Songea, aliendelea kupokea mishahara ya miezi mitano ya jumla ya shilingi milioni 23 baada ya kuacha kazi hiyo na kugombea ubunge wa jimbo la Makete.

Kwa mujibu wa Mwananchi, imebainika kuwa ofisa utumishi wa ofisi ya katibu tawala wa mkoa wa Ruvuma ndiye aliyemrudisha kwenye orodha ya malipo ya mshahara uleule wa ukuu wa wilaya wakati tayari ameshaachia nafasi hiyo.

Hivyo, mishahara miwili ililipwa kwa nafasi moja ya wakuu wa wilaya kwa kipindi cha miezi mitano, Profesa Sigalla anadaiwa kupokea kiasi cha shilingi milioni 4.6 kila mwezi.

Rais John Magufuli alianzisha msako wa watumishi hewa ulioibua madudu na hadi sasa zoezi la uhakiki linaendelea kuwatesa baadhi ya watumishi wa umma waliokuwa wakijipatia mishahara kinyume na sifa walizonazo.

Jurgen Klopp: Tunapaswa Kujilaumu Wenyewe
Ofisi ya chama cha Donald Trump yapigwa bomu la kienyeji