Mbunge wa Temeke kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Abdallah Mtolea ameipinga taarifa ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) wilayani Temeke ambayo ilieleza kuwa kiasi cha Shilingi milioni moja kiliokolewa baada ya kuidhinishwa kutolewa katika mfuko wa jimbo bila ya kuwepo kwa uthibitisho wake.

Amesema kuwa yeye ndiye mwenyekiti wa mfuko wa Jimbo la Temeke na kwamba chini yake hakuna jambo la aina hiyo ambalo limewahi kutokea, kwani fedha za mfuko hazitoki bila kuidhinishwa kwenye kikao cha kamati.

“Jimbo la Temeke ni langu, hakuna kitu kama hicho na hiyo ripoti walimhoji nani wakati mimi kama mwenyekiti wa mfuko wa jimbo sina taarifa? Mbona sijawahi kupata hata dokezo na hiyo hela iliyozuiwa iko wapi?”, amesema Mtolea.

Hata hivyo, Agosti 3, 2018 Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Temeke ilipokea jumla ya taarifa 458 yakiwemo malalamiko na vitendo vya rushwa kutoka kwa wananchi kwa kipindi cha miezi 12.

Zaidi ya shilingi milioni 62 zimeokolewa na kurejeshwa serikalini kufuatia udhibiti wa mianya ya rushwa ikiwemo milioni moja ya mfuko wa maendeleo ya jimbo kwa mujibu wa ripoti hiyo

AFA washindwa kuvunja mkataba wa Pep Guardiola
Pogba aanza kuaga Old Trafford, kulamba mkataba mnono Camp Nou