Mbunge wa Mlimba (CCM), Godwin Kunambi amemtaka Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi akalale gerezani ili ajue mateso wanayoyapata wafungwa.

Ameeleza hayo bungeni jijini Dodoma katika mjadala wa bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria na kubainisha kuwa Tanzania ina sheria nzuri isipokuwa utekelezaji wake ndio tatizo.

Kunambi amesema Waziri akitembelea magereza na kuondoka hakuna maana yoyote kwa madai kuwa hawezi kujua shida wanazopata wafungwa na mahabusu.

“Waziri anapopanga ziara ya kwenda gerezani asiende kuzunguka na kuondoka, nashauri akalale huko ili anapoondoka asubuhi atakuwa amejifunza juu ya kinachoendelea huko,” amesema Kunambi.

Aidha, Mbunge huyo ametoa mfano kwa baadhi ya makosa akidai ni madogo yenye kudhaminika lakini watu wamekuwa wakifikishwa mahakamani na kubambikiwa kesi za uhujumu uchumi.

Biden aionya China
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Aprili 29, 2021