Mbunge wa Jimbo la Rombo kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Joseph Selasini ameomba muongozo akitaka viti vya bungeni kukarabatiwa kwa kuwa viti hivyo ni vibovu na vinawapa shida wabunge.

Salasini ameyasema hayo kwenye kipindi cha Maswali na majibu huku muongozo wake ukiitaka serikali itoe majibu ni lini viti hivyo vitakarabatiwa ili kuwaondolea adha wabunge wakati wa vikao.

”Mh. Spika viti hivi tunavyokalia havipo kwenye hali nzuri kabisa, vimechakaa na havifanyiwi marekebisho na leo kiti changu kimenifinya makalio. Je ni lini vitafanyiwa ukarabati ?,” amesema Selasini

Hata hivyo, baada ya kuomba muongozo huo Spika wa Bunge, Job Ngudai amesema kuwa suala hilo limepokelewa na litatolewa ufafanuzi.

 

Liverpool yakanusha kujiuzulu kwa Zeljko Buvac
Ashikiliwa na polisi kwa tuhuma za mauaji