Mbunge wa Tandahimba (CUF), Katani Ahmed Katani (wa kwanza kushoto-pichani) jana alikana vikali taarifa iliyosambaa ikidai kuwa amehamia CCM.

Taarifa za Katani kuhamia CCM jana zilifuatana na taarifa za aliyekuwa Mbunge wa Temeke, Abdallah Mtolea kutangaza kujiuzulu kabla ya kukamilisha siku yake kwa kujiunga rasmi na CCM.

Katani alivitaka vyombo vya habari vilivyoanzisha na kuandika taarifa hiyo kumuomba radhi, huku akisisitiza kuwa kamwe hataondoka CUF.

“Sifikirii kujiuzulu leo, wala kesho na hata siku yoyote. Labda wanaotumika waje wanifukuze wenyewe,” alisema Katani.

Aidha, imeelezwa kuwa mwezi huu dirisha la wabunge wanaotaka kuhamia CCM litangwa rasmi na chama hicho tawala.

Video: Mawaziri vinara wa utoro Bungeni, Korosho kutoka Msumbiji zakamatwa Mtwara
Mama watoto wa Diddy akutwa amekufa kitandani, polisi wateta na Diddy

Comments

comments