Mbunge anayewakilisha jimbo la Rangwe nchini Kenya, Dkt. Lilian Gogo ‘ametoa mpya’ bungeni akipendekeza itungwe sheria ya kudhibiti watu wanaotoa ushuzi na kuchafua hewa ndani ya ndege.

Akichangia ndani ya Bunge hilo, mbunge huyo ameeleza kuwa harufu mbaya ya ushuzi ndani ya chombo hicho husababisha usumbufu mkubwa kwa abiria na inaweza kuwa chanzo cha kuhatarisha usalama.

Mchango wa mbunge huyo ulizua vicheko na kelele ya muda ndani ya nyumba hiyo ya wawakilishi wa wananchi wa Jamhuri ya Kenya.

“Ushuzi ni chanzo cha usumbufu kwa abiria ndani ya ndege japo hupuuzwa, na ni moja kati ya mambo yanayoweza kuhatarisha usalama, kuna abiria ambao hutoa harufu mbaya na kali baada ya kujamba,” Gogo anakaririwa na gazeti la Taifa Leo.

“Mbali na mikakati ya tiba ambazo zinaweza kupunguza kiwango cha gesi katika vyakula, inapaswa kutungwa sheria inayodhibiti aina ya vyakula wanayokula abiria wa ndege,” aliongeza.

Mbunge huyo alienda mbali akitaja ruti za Kisumu kwenda Nairobi kuwa ndizo ambazo zinaongoza kwa abiria kuachia ushuzi bila kujizuia wawapo ndani ya ndege.

Alipendekeza kuwa abiria wa ruti hizo wanapaswa kupewa dawa za kupunguza asidi tumboni lakini pia vyakula wanavyokula vinapaswa kudhibitiwa ili visiwe vinavyosababisha hali hiyo kwa kiwango kikubwa.

Katika hatua nyingine, Mbunge huyo aliitaka Serikali kuandaa muswada wa sheria ili upitishwe na bunge, unaodhibiti kiwango cha pombe wanazopewa abiria wa ndege.

Waziri Lugola amuonya Cyprian Musiba
Video: Serikali yatoa sababu gharama za vipimo Muhimbili kuwa juu