Mbunge wa jimbo la Chaani, Nadir Abdul amependekeza Serikali kuwasilisha Bungeni muswada wa sheria inayoruhusu adhabu ya kifo kwa watu wanaokutwa na hatia ya kubaka, ujambazi na kujihusisha na biashara za kulevya.

Abdul ametoa mapendekezo hayo Bungeni hivi karibuni alipokuwa akichangia mjadala wa Makadirio ya Bajeti ya Wizara ya Katiba na Sheria.

“Wabakaji, majambazi na wauza dawa za kulevywa wanapaswa kunyongwa hadi kufa. Hawa ni watu wabaya sana na Serikali inapaswa kuandaa sheria inayotamka adhabu ya kifo kwa watu wanaopatikana na hatia ya ubakaji, ujambazi na biashara ya dawa za kulevya,” alisema Mbunge huyo.

Aidha, Mbunge huyo pia alieleza kuwa ni wakati muafaka wa kuweka duka la kuuza bunduki visiwani Zanzibar kwani hivi sasa wazanzibar wengi wanalazimika kusafiri hadi jijini Dar es Salaam kununua silaha. Alisema kuwa yuko tayari kushirikiana na Serikali kuhakikisha duka hilo linaanzishwa kwani anaamini kuwa haitagharimu kiasi kikubwa cha fedha.

Inakadiriwa kuwa hadi sasa wazanzibar 130,000 wanahitaji bunduki za kawaida kwa ajili ya sababu za kiusalama.

kinondoni yatekeleza agizo la 10% kwa wanawake na vijana
Hello world