Spika wa Bunge, Job Ndugai leo Jumanne Juni Mosi, 2021 amemtoa katika ukumbi wa Bunge Mbunge wa Momba (CCM), Condester Sichwale kutokana na kuvaa suruali iliyombana.

Kwa mujibu wa kanuni za Bunge, wabunge wanawake hawaruhusiwi kuvaa suruali za kubana.

Mara baada ya kipindi cha maswali na majibu, alisimama Mbunge wa Nyang’wale (CCM), Hussein Amar na kuomba mwongozo wa Spika.

“Spika nasimama kwa kanuni ya 70 inayohusu mavazi ya staha kwa Wabunge, kanuni imeeleza wazi kuhusu mavazi hayo na kwa akina dada lakini humu ndani kuna Wabunge wamevaa nguo ambazo hazina staha,” amesema Amar.

Bonyeza link hapa chini kutazama Mbunge alivyotimuliwa bungeni

Minziro: Sina tatizo na Rais Karia
Rais Samia asimamisha kazi uongozi wa Kariakoo