Mwanasiasa mmoja nchini Uganda anayejulikana kwa jina la Ibrahim Abiriga ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana nchini humo.

Jeshi la Polisi nchini humo limesema kuwa mwanasiasa huyo wa Chama Tawala cha National Resistance Movement ‘NRM’ pamoja na mlinzi wake waliuawa karibu na makazi ya mwanasiasa huyo yaliyoko katika eneo linalojulikana Kawanda, Kaskazini mwa Jiji la Kampala.

Aidha, Abiriga mwenye umri wa miaka 62 ni Mbunge wa Arua na anajulikana kama mmoja wa wanasiasa waliokuwa mstari wa mbele kuunga mkono mswada wa kuondoa ukomo wa umri wa kugombea urais nchini Uganda.

Hata hivyo, Rais Yoweri Museveni amesema kuwa amesikitishwa na kifo cha mbunge huyo na kuagiza maafisa wa usalama kuwasaka waliomuua mbunge huyo.

Samia Suluhu aishika mkono Hospitali ya Mloganzila
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Juni 10, 2018