Mbunge wa Mbulu Mjini kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, Zacharia Isaay ameitaka Serikali ya Tanzania kueleza wazi kuhusu madai ya ugonjwa wa kupumua ambao anasema unamaliza watu wa jimboni mwake.

Isaay amezungumza Bungeni leo na kusema hawezi kuzungumzia Mpango wa Maendeleo wa Serikali badala yake anaona bora azungumzie hali ya Wananchi wake ambao kila mara anakwenda kuzika.

“Serikali iache kigugumizi Jimboni kwangu watu wanakwisha Spika. Nimechoka kuzika hata leo wanazika Mtoto wa Diwani wakati mwingine nashindwa kukuaga Spika kwenda Mbulu naamua kutoroka,” amesema Isaay.

Mbunge huyo amesema watu wanaopoteza maisha jimboni kwake  na magonjwa yao yanafanana ambayo ni tatizo la kupumua.

CORONA: CAF yaahirisha mchezo
Zahera: Ninaipa Simba 60%, AS Vita Club 40%