Mbunge wa Jimbo la Siha kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Godwin Mollel amesema kuwa tukio la kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu ulikuwa ni mpango wa (CHADEMA).

Amesema kuwa CHADEMA waliamua kumpiga risasi Tundu Lissu kwa kuwa alionekana anatengeneza umaarufu binafsi na wao wanataka kuuza nchi ndipo walipotumwa watu ambao wamemsababishia majeraha hayo.

Dkt. Mollel amesema kuwa katika mabomu ya Arusha yeye alikuwa ni Daktari aliyeiwakilisha CHADEMA kwenye Post moterm na alipotoka aliwataarifu viongozi wenzake juu ya sampuli alizoziiba na kutaka zipelekwe nchi ya Afrika Kusini lakini viongozi hao hawakuzifanyia kazi.

“Mimi nilikuwa huko lakini nilikimbia kwa mipango yao,” amesema Dkt. Mollel.

Aidha, kwa upande wao wabunge, Frank Mwakajoka (Tunduma) na Joseph Selasini (Rombo), kwa nyakati tofauti waliomba kutoa taarifa kuhusu hoja ya Mollel ambapo walimtaka mbunge huyo kuthibitisha kauli zake na kutovunja kiapo chake cha udaktari.

Akijibu kuhusu taarifa hiyo, Dkt. Mollel amedai kuwa ili athibitishe anataka Chama wanachotoka wabunge hao (CHADEMA) waeleze wanakopeleka ruzuku za chama hicho.

Hata hivyo, Dkt. Mollel alikuwa ni mbunge wa CHADEMA na baadaye kuhamia CCM ambako aligombea tena na kurejea bungeni akiwa amebadili chama, ameliambia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa yeye aliiba sampuli ambazo chama hicho kilimkataza kuzitumia.

Wasafirishaji wa Mirungi wageuka kuwa Wanafunzi
Wananchi wa Kijiji cha Nandete wajitolea kujenga Zahanati