Mbunge wa Jimbo la Kilwa Kusini, Selemani Bungara (Bwege) ametangaza kukihama Chama cha ‘Civic United Front (CUF)’ na kuhamia Chama cha ACT-Wazalendo mara baada ya Bunge kuvunjwa kesho.

Amesema kuwaamejiridhisha na jahazi la ACT wazalendo na Bunge likimaliza muda wake atajiuzuru na kuhamia kwenye chama hicho.

”Nimejiridhisha kuwa ACT Wazalendo ni jahazi sahihi la kupigania demokrasia, haki na maendeleo ya Watanzania” amesema Mbunge Bungara.

Ameongeza kufafanua ”nimeitumikia nafasi ya uwakilishi wa wananchi kwa maana ya ubunge wa Kilwa Kusini kwa vipindi viwili mfululizo kupitia CUF Chama cha wananchi, hivyo sina budi kukishukuru chama changu kwa kunifikisha hapa nilipo na naahidi hapa kuwa sitokisahau kamwe katika maisha yangu yote”.

Na kuiongeza “niliipenda sana CUF kwa mapambano yake ya kupigania haki sawa kwa wote, ninasikitika sana kuwa CUF ya sasa imeacha mapambano hayo yaliyoijengea heshima na imani kubwa ya wananchi”

Ndugai amtaja Bernard Morrison Bungeni
Sera za Nyalandu na Mchungaji Msingwa Wanavyoutaka Urais 2020