Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Ruvuma, Jackline Ngonyani (CCM) juzi alinusurika kupigwa na wabunge wa viti maalum wa kambi ya Ukawa kutokana na makombora aliyowarushia bungeni.

Wabunge hao wa Ukawa walimfuata Ngonyani nje ya Bunge baada ya kumalizika kwa kikao cha bunge juzi, kutokana na kauli yake ya kudai kuwa wabunge wanawake wa kambi ya Ukawa ni madebe matupu yanayopiga kelele isipokuwa wawili tu ambao ni Magdalena Sakaya (CUF) na Mbunge wa Viti Maalum, Upendo Pendeza (Chadema).

Kauli hiyo ilizua tafrani, wabunge wa Ukawa walisimama kupinga bungeni lakini hawakuweza na Mbunge huyo aliendelea kuwapa ‘dozi’ ya vijembe aliyoiandaa kwa ajili yao.

Mashuhuda wa tukio hilo wameeleza kuwa juzi wabunge hao wa viti maalum wa Ukawa walimfuata Nyonyani nje ya Bunge baada ya kuahirishwa kwa kikao kwa kasi kabla ya kuwaponyoka.

“Njoo… usikimbie subiri hapo hapo, mbona unakimbia… na bahati yak oleo tungekuonesha adababu hapahapa,” anakaririwa Mbunge wa wa Viti Maalum Mkoa wa Kigoma, Sabreena Sungura.

Ngonyani alipoulizwa na gazeti la Mtanzani kuhusu sakata hilo, alikiri kutokea na kueleza kuwa yeye hapigiki.

“Ninachokwambia hapigwi mtu hapa. Mle ndani ni kujenga hoja sio ngumi. Mimi nilitoka baada ya Bunge kuahirishwa sasa kuna watu walitaka kunipiga hilo mimi silijui na wao (Ukawa) ndio wanaolikuza,” alisema Ngonyani.

Zitto, Halima Mdee, Heche wahojiwa kwa kufanya fujo bungeni
Lowassa, Sumaye watajwa sakata la uuzwaji nyumba za serikali, Mbowe alipua