Mbunge wa Jimbo la Ndanda kupitia tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe amesema kuwa anayekwamisha Tanzania ya Viwanda ni Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Ameyasema hayo Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akichangia hoja katika bajeti ya wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji mwaka 2018/19.

Katika mchango wake Mwambe amesema kuwa, Waziri Mwijage atakapohitimisha hoja ya bajeti anatakiwa aeleze kuwa wawekezaji waliosajiliwa mwisho wao huwa ni upi, ambapo amesema kusajili ni jambo jingine na kuendesha ni shughuli nyingine.

“Aliyetufikisha hapa ni Waziri Mwijage, kila akisimama yeye anasema ni mzee wa ‘porojo’ na wanao msaidia wanasema wanapaswa kuwa wazee wa porojo,”amesema Mwambe

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Liwale kupitia Chama Cha Wananchi (CUF), Zuber Kuchauka amesema kuwa bado mazingira ya uwekezaji ni magumu na si rafiki kitu ambacho kinawafanya wawekezaji kukimbilia nchi nyingine.

 

 

 

Msichana aliyemuua mumewe aliyekuwa anambaka ahukumiwa kifo
50 Cent ajiondoa Instagram, adai wamemuudhi