Mbunge wa Moshi Vijijini kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Anthony Komu ametoa msimamo wake unaotofautiana na Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kuhusu kususia uchaguzi wa majimbo matatu unaotarajiwa kufanyika mwakani.

Mbowe alisema kuwa kama Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) haitaahirisha uchaguzi huo uliopangwa kufanyika januari 13 mwakani ili kushiriki majadiliano, hawatashiriki uchaguzi huo, lakini Komu amesema kuwa kufanya hivyo ni kosa kubwa ambalo linaweza kuwaathiri katika chaguzi zijazo.

“Hatuko sahihi kususia uchaguzi haya ni mapambano ya vita, na unatakiwa kuangalia wapi ulipokosea ili ujisahihishe, hata hizo Kata 43 hatukuonewa, ndiyo maana tulipata Kata moja tu ambayo tulijipanga,”amesema Komu

Aidha, Mbunge huyo amesema kuwa uamuzi huo wa kususia uchaguzi unazua maswali mengi, kwani kufanya hivyo kutatoa faida kubwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kupata ushindi katika majimbo yote.

Video: JPM atangaza kiama wanaovaa nusu uchi
Magazeti ya Tanzania leo Desemba 13, 2017