Mbunge wa Wawi (CUF), Ahmed Ngwali ameitaka serikali kukiri wazi kwamba imeshindwa kuzuia uingizwaji wa bidhaa bandia nchini licha ya jitihada ambazo serikali inatangaza kuzifanya lakini bado bidhaa hizo zimeeendela kuingia  nchini.

Ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma wakati wa kuchangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji kwa mwaka wa fedha 2018/2019 na kuongeza kuwa polisi ndiyo watuhumiwa wakubwa katika uingizwaji wa bidhaa hizo.

“Serikali iseme tu kama imeshindwa kuzuia bidhaa bandia nchini,  lakini polisi ambao unasema katika kitabu chako,  mnataka kutumia mpaka Interpol katika kuzuia bidhaa feki, polisi hao wenyewe ndiyo wanashiriki katika mambo hayo ya kuingiza bidhaa feki, sasa hiyo Interpol gani mnataka kutumia? Mheshimiwa Mwijage hilo mlirekebishe” amesema Ngwali.

Aidha, Ngwali ameongeza kuwa serikali imekua inatumia mifumo mbalimbali ikiwemo ukaguzi wa mizigo bandarini lakini tatizo la uingizwaji wa bidhaa bandia umeendelea kuwa mkubwa.

Hata hivyo, kwa upande mwingine Mbunge huyo amesema mahitaji ya gypsum nchini ni makubwa kuliko uwezo wa uzalishaji wa viwanda vya ndani ambavyo vipo vinne tu na vina uwezo wa kuzalisha gypsum milioni tano tu wakati mahitaji ya gypsum nchini ni zaidi ya milioni 10 hadi 12

 

Video: Serikali ya JPM yapewa darasa zito la Viwanda, Dkt. Slaa awapa wapinzani mbinu kwa Rais Magufuli
Magazeti ya Tanzania leo Mei 13, 2018