Mbunge wa Nakuru Mjini Mashariki, David Gikaria ametiwa mbaroni kwa madai ya kuwashambulia wapiga kura.

Kamanda wa polisi kaunti ya Nakuru, Peter Mwanzo amethibitisha kukamatwa kwa mbunge huyo na kusema anatuhumiwa kumvamia na kumjeruhi mpiga kura katika kituo cha kupigia kura katika eneo la jimboni kwake.

Gikaria alikamatwa katika kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi ya Naka kufuatia ghasia aliyoifanya akiwa katika eneo hilo.

Mbunge wa Nakuru Mjini Mashariki, David Gikaria. (picha na Nation Media)

“Tulimkamata baada ya kumvamia na kumjeruhi mpiga kura na pia amezua tafrani na fujo katika kituo cha kupigia kura na hatutakubali hilo,” amesema Mwanzo.

Mpiga kura huyo aliyeshambuliwa alilazwa hospitalini akiwa na majeraha kichwani.

Gikaria anazuiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi cha Nakuru.

Mabadiliko Uwanja wa Mkapa, mashabiki walalamikiwa
Kizz Daniel aeleza sababu kutopanda jukwaani