Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael na Meya wa Mji huo, Raymond Mboya (Chadema), walijikuta wakiishia getini katika Ikulu ndogo mkoani kilimanjaro mara baada ya kuzuiliwa kuonana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli alipowasili mkoani humo.

Aidha, hatua hiyo ilifikiwa mara baada ya kutokuwepo kwa taarifa zao kuhusu kuonana na Rais Dkt. John Magufuli.

“Ni kweli niliondolewa kwenye foleni, alikuja Ofisa usalama mmoja akaniambia kistaarabu kuwa mimi sikuwa nahitajika katika kikao hicho, nilijaribu kumwambia kuwa mimi ni mbunge lakini akasisitiza kuwa sihitajiki,”amesema Michael.

Kwa upande wake Meya wa Moshi Mjini, Raymond Mboya amesema kuwa alipewa taarifa na viongozi wa Halmashauri na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuwa wanahitajika katika kikao hicho cha Rais Dkt. Magufuli ambacho kilipangwa kwaajili ya kukutana na viongozi wa dini.

Hata hivyo, Rais Dkt. John Magufuli yuko Mkoani Kilimanjaro kwa ajili maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani.

Video: Serikali kuboresha maslahi ya wafanyakazi
?Live: Yanayojiri Moshi katika maadhimisho siku ya wafanyakazi Duniani

Comments

comments