Mbunge wa Geita Joseph Musukuma leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama Hakimu Mkazi Geita, kujibu tuhuma zinazomkabili, baada ya kushikiliwa na polsi tangu jumapili ya wiki iliyopita.

Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Geita, Mponjoli Mwabulambo ambapo amethibitisha kumpeleka Mahakamani mbunge huyo, ambaye anatuhumiwa kuhusika na kuratibu vurugu katika mgodi wa GGM mkoani humo.

“Wamepelekwa Mahakamani asubuhi hii amesema Kamanda wa polisi wa mkoani Geita,” amesema Kamanda Mponjoli Mwabulambo

Hata hivyo, Mbunge Musukuma pamoja na baadhi ya wadiwani na wananchi, walikamatwa na polisi kwa kufunga njia inayoeleka kwenye mgodi wa GGM na kuleta vurugu, kushinikiza mgodi huo kulipa dola milioni 12.

Video: Diamond afunguka kuhusu mtoto wa Hamisa Mobeto
Aliyezuia vita vya nyuklia wakati wa vita baridi afariki dunia