Mbunge anayewakilisha Kiambu nchini Kenya, Gathoni Wamuchomba amewataka wanaume wenye uwezo kutoka jamii ya Kikuyu kufikiria kuoa wanawake wengi ili kutatua baadhi ya matatizo katika jamii hiyo.

Wamuchomba ameeleza kuwa kwakuwa katika jamii hiyo kumekuwa na tatizo la wanawake wengi kulea watoto wakiwa peke yao huku wanaume wakizaa na wanawake tofauti, ndoa ya mitala itakuwa sehemu ya utatuzi wa changamoto hiyo.

Alisisitiza kuwa wanaume wenye waliozaa nje ya ndoa wanapaswa kuwaoa pia wanawake hao kwani kuoa wanawake wengi sio kosa bali ni sehemu ya tamaduni za kiafrika.

“Tunawazaa hawa watoto na hatutaki kuwamiliki. Kama wewe ni mwanume kutoka jamii ya Kikuyu, na unaweza kuwatunza wanawake watano, waoe wote kama unao uwezo wa kulea watoto wengi,” alisema.

Kwa mujibu wa Daily Nation, mbunge huyo alisema kuwa tatizo la ulevi wa kupindukia pamoja na matumizi ya dawa za kulevya kwa vijana wengi linatokana na kukosa malezi bora.

Alisema watoto wengi wa mitaani ni zao la kukosa malezi ya wazazi wawili husan mama zao kukosa fedha za kuwahudumia.

 

 

JPM afanya uteuzi wa Mkemia Mkuu wa Serikali
Waliomteka Padri wadai pesa kumuachia

Comments

comments