Upepo wa kutumbuliwa jipu, jana ulielekezwa kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mwigulu Nchemba.

Upepo huo ulielekezwa kwa mawaziri hao na Mbunge wa Bukoba Vijijini, Jasson Rweikiza (CCM) ambaye aliwanyooshea kidole mawaziri hao kwa kushindwa kutekeleza ahadi ya Rais, John Magufuli ya kuondoa tozo zisizo na tija kwenye mazao hususan Kahawa inayolimwa kwa wingi jimboni kwake.

“Sasa ni miezi takribani sita tangu tangu mteuliwe na kodi hizi bado zinaumiza wakulima na hamjazifuta. Je, hamuoni kuwa ni heri Rais atomize ahadi yake kuwatumbua kwa kuchelewa kutekeleza ahadi yake?” Rweikiza alihoji.

Hata hivyo, Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Nchemba alitoa majibu akimueleza mbunge hyo kuwa wizara hiyo iko katika hatua za mwisho za maadilizi ya muswada wa sheria ya makato na kodi na itauwasilisha Bungeni hapo hivi karibuni kwa ajili ya kupitishwa, ili ahadi ya Rais iweze kutekelezwa kwa kuondoa kodi na tozo zinazoudhi kwa wakulima.

Meya Kinondoni abaini ujenzi wa barabara hewa kwa zaidi ya milioni 300
Ukawa wamuweke mtego Maghembe, wamtwisha zigo la hasara ya shilingi bilioni 3

Comments

comments