Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokea Zanzibar, Zainab Mussa Bakari amepata ajali katika eneo la Dumila mkoani Morogoro alipokuwa akitokea jijini Dodoma mara baada ya kuahirishwa kwa vikao vya bunge.

Taarifa ya ajali hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CHADEMA, Tumaini Makene ambapo amesema kuwa Mbunge huyo anatarajiwa kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kupatiwa matibabu zaidi.

“Mbunge wa CHADEMA (VM) Zanzibar, Bi. Zainab Mussa Bakari amepata ajali eneo la Dumila akitoka Dodoma leo, abiria wote 3 na dereva wamejeruhiwa, baada ya kutibiwa kwa dharura Morogoro, sasa wanapelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili1 kwa uchunguzi na matibabu zaidi,” amesema Makene

Hata hivyo, Mapema jana, mmoja wa viongozi wa juu wa chama hicho, Waziri Mkuu Mstaafu Fredrick Sumaye alihamishiwa hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya kuzidiwa alipokuwa kwenye majukumu ya kikazi mkoani Tanga.

 

Video: Makamu wa Rais aongoza kikao cha kujadili masuala ya Muungano
Sababu yatajwa wanaume wenye umri mdogo kutunga mimba haraka wanawake wenye umri mkubwa