Mahakama ya wilaya ya Kilombero imemuhukumu kwenda jela miezi sita Mbunge wa jimbo la Kilombero, Peter Lijualikali (30) kwa kosa la kufanya fujo na kusababisha taharuki katika maeneo ya ukumbi Wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.

Mwendesha mashtaka inspekta wa Polisi Dotto Ngimbwa aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa, akiwa mshtakiwa namba moja pamoja na mwenzie Stephano Mgata (35) walitenda kosa hilo machi mosi mwaka 2016 kwenye kikao cha Baraza la Madiwani katika eneo la Kibaoni ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilombero.

Kufuatia ushahidi uliotolewa mahakamani hapo, Hakimu mkazi katika mahakama ya wilaya ya Kilombero Timothy Lyon aliwatia hatiani washtakiwa hao walipatikana na makosa. Aidha, Hakimu alisema kuwa mshtakiwa wa kwanza ambaye ni Mbunge ambaye alikuwa na kesi tatu huko nyuma atatumika kifungo cha miezi sita jela kwa kuwa anaonekana kuwa mkosaji mzoefu.

Hata hivyo Mahakama hiyo imeona kwa kuwa mshtakiwa wa pili Stephano Mgata (35), hili ni kosa lake la kwanza amehukumiwa kifungo cha miezi sita nje ambapo ndani ya kipindi hicho cha miezi sita hatotakiwa kutenda kosa lolote la jinai.

Video: Maneno ya Diamond kuhusu kutumbuiza AFCON 2017 Gabon
Majaliwa ataka miradi inayojengwa iendane na thamani