Mbunge wa jimbo la Liwale (CUF), Zuberi Kuchauka amejivua uanachama wa CUF na nyadhifa zake zote na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).

Amechukua uamuzi huo jijini Dar es salaam ambapo amepokelewa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Bashiru Ally.

Amesema kuwa amekuwa akishindwa kutimiza majukumu yake kufuatia migogoro iliyodumu kwa muda mrefu ndani ya Chama Cha Wananchi (CUF)

“Nadhani kila mtu kwasasa ukimwambia wewe ni mwanachama wa Chama Cha Wananchi CUF, atakuuliza CUF ya nani Maalim Seif ama Prof. Lipumba, sasa kitu kama hicho si kizuri ni bora kuchagua moja kuwa wa moto au baridi kuliko kuwa vuguvugu, yaani hueleweki,”amesema Kuchauka

Hata hivyo, ameongeza kuwa ameamua kuchukua uamuzi huo ili kuunga mkono jitihada na juhudu zinazofanywa na Rais Dkt. Magufuli za kuleta maendeleo katika jamii.

Majaliwa awataka viongozi wabadilike kimtazamo
Rais Magufuli afanya teuzi mpya zaidi ya nafasi 41

Comments

comments