Mbunge wa ngome ya upinzani ya NASA, Stephen Mule anayewakilisha jimbo la Matungulu amemtaka kiongozi wa ngome hiyo, Raila Odinga kuacha kuwaweka Wakenya ‘rehani’, akubali kuzungumza na Rais Uhuru Kenyatta kwa maslahi ya nchi.

Mule alimtaka Raila kutambua kuwa muda unazidi kwenda huku wabunge wa NASA wakiwa nje ya Bunge hivyo kushindwa kufanya kazi yao ya kikatiba ya kuisimamia Serikali.

Stephen Mule

“Hayo hayatatusaidia. Wanajeshi wa miguu ndani ya bunge hawawezi kuendelea kutembea nje ya bunge wakati wanapaswa kuwa ndani kuisimamia Serikali. Naamini Mungu yuko upande wa nchi hii. Kama nchi haikuteketea Januari 30, haitateketea kamwe,” Mule ananukuliwa.

Alisisitiza kuwa Raila na Uhuru wanapaswa kuwekana sawa, kukaa mezani na kuzungumza ili nchi isonge mbele.

Katika hatua nyingine, aliitaka Jubilee kuheshimu maamuzi ya Mahakama na kufuata sheria.

Alikumbusha kuwa ni Mahakama ile ile iliyothibitisha ushindi wa Rais Kenyatta, hivyo wanapaswa kuisikiliza na kuiheshimu inapotoa uamuzi mwingine pia.

Wolper: Tanzania jina la nchi yetu naona si tamu tena na limeanza kuwa chungu
Video: Mauaji ya mwanachuo yavuruga Polisi, Wazazi watoa neno zito