Mbunge Jimbo la Nyamagana mkoani Mwanza Mhe. Stanslaus Mabula ametoa pongezi hizo kwa Wananchi wa Mtaa wa Nyakamanga kwenye ziara yake ya Mtaa kwa Kata Katika Kata ya LWANIMAH wakati akikagua ujenzi wa soko la NYAKAMANGA lililojengwa kwa nguvu za Wananchi.

Mhe. Mabula amesema kuwa, haijawahi kutokea Mtaa kuwa na mradi wake wenyewe bila nguvu ya halmashauri ya Jiji au serikali kuu.

Hivyo ametumia hadhara hiyo kutoa wito kwa mitaa mingine kujifunza kwa Wana NYAKAMANGa na kuahidi kupeleka taarifa hizo TAMISEM ili ichukue mfano wa ubunifu huo.

Soko la Nyakamanga linatarajiwa kuwa na ofisi za serikali ya Mtaa, Ukumbi wa Mikutano, Maduka n kuhifadhi Wachuuzi wapatao 100 ambao watahudumia Kaya 400 zenye wananchi takribani 1500 Hadi 200.

Katika ziara hiyo Mhe. Mabula aliambatana na Mwenyeji wake Diwani Kata ya Lwanimah, Mwenyekiti Mtaa wa Nyakamanga Ndg. Joseph Charlse, Mjumbe Kamati ya siasa CCM Nyamagana Comrade Sanyenge pamoja na Katibu wa UVCCM wilaya ya Nyamagana Comrade Malanyingi Matukuta, Viongozi waandamizi wa CCM Kata wakiongozwa na Mwenyekiti Kata na Kamati yake ya siasa.

PICHA: Mabingwa ASFC waanza safari ya Dar es salaam
Waziri Biteko: Marufuku kuchimba 'DHAHABU' mlima Kaputa