Mbunge wa Shinyanga Mjini (CCM), Stephen Masele amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP).

Taarifa hiyo imetolewa Mei 11, 2018 bungeni mjini Dodoma na Mwenyekiti wa Bunge, Andrew Chenge na kubainisha kuwa mbunge huyo kijana amechaguliwa jana kwa kura nyingi.

“Umelipa Bunge letu sifa na Tanzania kwa ujumla. Nafasi hii ni ya kuitangaza nchi yetu na Bunge hili tunamtakia kazi njema,” amesema Chenge ambaye pia ni Mbunge wa Bariadi kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

“Nampongeza sana kijana huyu, lakini pia Serikali kwani huwezi kupata nafasi hii kubwa kama huungwi mkono na Serikali. Nimpongeze sana,”pongezi kutoka kwa Rais John Magufuli.

Makomando wa Marekani wawakamata Al-Shabaab
Angalia video ya wimbo mpya wa Ali Kiba, 'Mvumo wa Radi'