Mbunge wa viti maalum wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wa Mkoa wa Singida, Jesca Kishoa amepata ajali Jijini Dodoma.

Afisa Habari wa CHADEMA, Tumaini Makene amesema kuwa, Kishoa amepata ajali asubuhi kwa kugongana na gari ndogo aina ya Pick Up alipokuwa njiani akielekekea kwenye majukumu yake ya kibunge.

Amesema kuwa kwa sasa Kishoa yupo katika Zahanati ya Bunge akipatiwa matibabu na uangalizi wa awali na kwamba wanasubiri kupata taarifa za Madaktari ili kujua hatua zaidi.

Kwa upande wake Mume wa Mbunge huyo, aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila amesema kuwa amepata taarifa za ajali hiyo ya mkewe na kwasasa yupo Morogoro akielekea Jijini Dodoma kwa ajili ya kumuona mkewe.

Fahamu makosa 5 yanayofanyika wakati wa kununua gari
Ali Kiba afunguka kufikishwa mahakamani akidaiwa matunzo ya mtoto 

Comments

comments