Mbunifu mahiri na maarufu wa mavazi kutoka nchini Marekani, Virgil Abloh (41) amefariki Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ndugu zake kupitia ukurasa wake wa mtandao wa instagram, imebainisha wazi sababu za kifo cha Virgil kuwa ni maradhi ya saratani aliyokuwa akikabiliana nayo kwa kupindi cha zaidi ya miaka miwili.

Virgil Abloh enzi za uhai wake alikuwa mkurugenzi wa Idara ya ubunifu wa Louis Vuitton Campany kwenye eneo la mavazi ya kiume ambapo amehudumu kwa kipindi cha miaka minne tangu alipojiunga rasmi na kampuni hiyo mapema mwaka 2018.

Nje ya hapo Abloh alikuwa Mkurugenzi wa kampuni yake binafsi ya mavazi iitwayo Off-White aliyoifungua rasmi mnamo mwaka 2012.

Kitaaluma marehemu Abloh alikuwa mbobezi wa usanifu majengo ‘Architect’ na alijitumbukiza rasmi kwenye tasnia ya ubunifu wa mavazi mnamo mwaka 2019 kwa kuanza kufanya kazi na kampuni ya mavazi ‘Fendi’.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 29, 2021
Rekodi ya kuvaa gauni la harusi refu zaidi duniani