Mbwa mmoja katika jimbo la Minnesota, Marekani amechaguliwa tena kuwa  meya  jimbo hilo.

Mbwa huyo anayejulikana kwa jina Duke ana umri wa miaka tisa na alichaguliwa mara ya kwanza kuwa meya wa mji wa Cormorant mwaka 2014, kwa mujibu wa kituo cha habari cha WDAY kituo ambacho kina ushirikiano na shirika la habari la ABC.

Wadhifa wa meya wa Cormorant huwa wa staha na watu huhitajika kulipa dola moja ili waruhusiwe kupiga kura.

Mmiliki wa mbwa huyo David Rick aliwaambia wanahabari kwamba mara ya kwanza mbwa huyo kuchaguliwa ilikuwa kibahati lakini baadaye ameibukia kupendwa sana na wakazi.

Mji huo, ambao kwa mujibu wa ABC News ulianzishwa 1874, kwa sasa una wakazi takriban 1,000.

Kuchaguliwa kwa Duke kuwa meya wa Cormorant miaka miwili iliyopita kulitokea siku chache baada ya kujiuzulu kwa aliyekuwa meya wa mji jirani wa Dorset, Robert Tuff.

Duke si mnyama wa kwanza kuchaguliwa kuongoza. Miaka karibu 20 iliyopita, paka anaejulikana kwa  jina la Stubbs alichaguliwa kuwa meya wa mji wa Talkeet katika jimbo la Alaska.

 

Watu Sita Wafariki Kutokana Na Tetemeko la Ardhi Italia
Wapenzi Wa Jinsia Moja Wajifungua Watoto Watatu Afrika Kusini