Mbwana Samatta, Mshambuliaji wa Klabu ya KRC Genk na nahodha wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), jana, Januari 17, 2019 alitua jijini Birmingham kwa ajili ya zoezi la vipimo vya afya yake ikiwa ni hatua ya kuelekea kusaini mkataba wa kuichezea Klabu ya Uingereza ya Aston Villa.

Mbwata ambaye alikuwa mchezaji wa kwanza wa Tanzania kufunga goli kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Barani Ulaya, alipoifunga Liverpool FC akiichezea klabu yake ya KRC Genk, sasa anatarajiwa kuwa Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Uingereza ambayo ni ligi ya soka maarufu zaidi duniani.

Baba yake Mbwana, Ally Pazi Mbwana alizungumza na gazeti la Mwananchi na kueleza kuwa mwanaye alimpigia simu asubuhi na kumueleza kuwa anaelekea Birmingham kwa ajili ya vipimo, zoezi litakalofanyika leo.

“Mwanangu alinipigia simu leo asubuhi, akaniambia kuwa yuko uwanja wa ndege anasafiri kuelekea Birmingham kukamilisha taratibu za mkataba wake mpya ikiwa ni pamoja na kufanya vipimo,” alisema Mzee Pazi.

Kwa mujibu wa BBC, Mbwana anatarajia kusaini mkataba mnono wa £10 Milioni, ikiwa ni hatua ya Kocha wa Aston Villa, Dean Smith kuboresha safu ya ushambuliaji.

Video: Lukuvi ashitukia dili, Utajiriwa wa MO waporomoka kwa dola milioni 300
Iran: Kiongozi Mkuu wa kidini alikingia kifua jeshi kudungua ndege ya abiria