Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine kesho Jumatano anatarajiwa kuongozana na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania na klabu ya TP Mazembe ya Congo DR, Mbwana Samatta kuelekea nchini Nigeria kwenye sherehe za utoaji wa tuzo kwa wachezaji bora barania Afrika.

Mwesigwa anatarajiwa kuondoka na Samatta kuelekea Nigeria katika mji wa Abuja ambapo sherehe za utoaji tuzo hizo zitafayika  Alhamisi Januari 7, ambapo siku ya sherehe hizo Katibu Mkuu ataambatana na Ofisa ubalozi wa Tanzania nchini Nigeria

Mbwana Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani, huku pia akiwa mfungaji bora wa michuano ya Ligi ya Mabingwa (CAF CL) baada ya kuifungia klabu yake ya TP Mazembe mabao 8 na kuibuka mabingwa wapya wa michuano hiyo.

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amemtakia kila la kheri Mbwana Samatta katika kinyanganyiro hicho cha uchezaji bora na kusema kwa niaba ya watanzania wote wanamuombea dua njema aweze kuibuka mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani.

Samatta anawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika pamoja na mlinda mlango wa TP Mazembe, Robert Kidiaba (Congo DR) na mshambuliaji wa Etoile du Sahel Baghdad Boundjah (Algeria).

Chris Gayle Aadhibiwa Kwa Kumtongoza Mwanahabari
Chelsea Na Man Utd Zawania Saini Ya Beki Wa Kibrazil