Nahodha na mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Mbwana Samatta amekiri kuwa na maumivu kwa kuwa alicheza mfululizo akiwa na klabu yake ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Jana uongozi wa klabu ya Genk ulitoa angalizo kwa maafisa wa shirikisho la soka nchini TFF juu ya kumtumia mshambuliaji huyo wakidai ametumika mfululizo.

Licha ya kukiri kuwa na maumivu, Samatta ameahidi kuwasiliana na daktari wa Taifa Stars ili kuona njia salama ya kufanya bila kumletea madhara.

“Nimefika salama, ni kweli nilikuwa na maumivu kwa sababu nilicheza mechi mfululizo, nafikiri tutawasiliana na daktari wa Taifa Stars kabla ya kucheza ili tuone tunafanyaje kabla ya kucheza ili isilete madhara” alisema Samatta.

Mchezo wa Stars dhidi ya Nigeria utakuwa ni wa kukamilisha ratiba kwa timu zote mbili kwa kuwa hazina nafasi ya kufuzu kwa Afcon mbele ya kinara wa kundi lao Misri.

Mapokezi ya Waziri Mkuu Mjini Dodoma leo Yaahirishwa
Kweli Ng'ombe Wa Masikini Hazai, Shkodran Mustafi Aumia