Emmanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili anashikiliwa na jeshi la polisi katika kituo cha polisi Mabatini kilichopo kijitonyama Jijini Dar es salaam tangu Mei 2 mwaka huu kwa kosa la kutumia mtandao wa You Tube bila kujisajili.

Polisi wameeleza kuwa MC Pilipili hajasajili akaunti yake ya YouTube na kulipa ada kwa mujibu wa kanuni za TCRA.

Na mapema leo anaweza kupandishwa mahakamani kujibu shitaka linalomkabili.

Mamlaka ya mawasiliano Tanzania mwaka jana ilitoa muda kwa wamiliki wa blogu kusajili mitandao yao chini ya sheria lengo likiwa kudhibiti maudhui ya mitandao hiyo.

Ambapo ilipitishwa kwa kila mmiliki wa televishini mtandaoni, chaneli ya you tube kulipa milioni 1 ili kupata leseni ya kuendesha shughuli hizo.

Sheria hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya 4 ya Maudhui Mtandaoni ya mwaka 2018 ( The electric postal Communications online content, Regulations 2018) ambapo TCRA imepewa dhamana ya kuandaa na kutunza rajisi ya watoa huduma za maudhui kupitia blogu, majukwaa mtandaoni, radio na televisheni za mtandaoni.

Aidha, adhabu ya kukiuka sheria hiyo ilikuwa ni pamoja na kulipa faini ya isiyopungua dola 2000 sawa na Milioni 4 na zaidi kwa pesa ya kitanzania au kufungwa jela kwa muda usiopungua mwaka mmoja au kutumikia adhabu zote kwa pamoja.

Je unatafuta ajira?, Hizi hapa nafasi 10 za ajira kwa ajili yako
LIVE: Mwili wa Dkt. Reginald Mengi ukiagwa wakati huu Karimjee

Comments

comments