Bingwa wa mapigano ya UFC, Conor McGregor amemjibu bingwa wa zamani wa masumbwi ya uzito wa juu, Mike Tyson kuhusu kauli yake kuwa mpiganaji huyo atakufa kwenye pambano kati yake na Floyd Mayweather.

McGregory ambaye anajiandaa na pambano hilo litakalofanyika Agosti 26 mwaka huu nchini Marekani amemkejeli Tyson kwenye post nyingine kuwa yeye ndiye Don King mpya na kwamba atakula maneno yake. Ikumbukwe kuwa Don King alikuwa promota maarufu aliyefanya biashara kubwa ya mapambano ya Tyson.

“Mtakula maneno yetu katika siku zote za maisha yenu, wakati huo mimi nakula samaki (lobster) kwa maisha yangu yote,” tafrisi isiyo rasmi ya alichoandika McGregor kwenye picha aliyoweka Instagram inayoonesha anafanya mazoezi kujiandaa na pambano hilo.

You are all going to eat your words for the rest of your days, while I eat lobster for the rest of mine.

A post shared by Conor McGregor Official (@thenotoriousmma) on

Katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, Tyson alisema kuwa McGregor ataambulia kifo kwa knockout kwani Mayweather amekuwa akipigana masumbwi tangu akiwa mdogo hivyo hawezi kupigwa tena kwa mara ya kwanza na mtu ambaye hajawahi kushiriki mchezo huo.

Pambano la Mayweather na McGregor linatarajiwa kuvunja rekodi ya mapato ya mapambano ya masumbwi. McGregor anatarajia kuingiza zaidi ya dola za kimarekani milioni 100.

Inatarajiwa kuwa watu watakaoangalia pambano hilo kwenye mfumo wa Pay-per-view watazidi idadi ya watu milioni 4.4 iliyoshuhudiwa katika pambano la mwaka juzi kati ya Mayweather na Manny Pacquiao.

Spika Ndugai aridhia kuvuliwa uanachama Wabunge 8 CUF
Wanaosababisha hoja za ukaguzi wachukuliwe hatua - RC Rukwa