Mbunge wa Iringa Mjini kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mch. Peter Msigwa amesema kuwa baadhi ya vingozi hasa wakuu wa mikoa wanaongoza kwa mihemko ya kisiasa kitu ambacho kinapunguza ufanisi  katika utendaji kazi kwa watumishi umma.

Ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati akichangia kwenye mjadala juu ya utawala bora ambapo amedai kuwa baadhi ya wateule mkoani kwake wanatumia vibaya mamlaka yao ya kisheria.

“Mara nyingi tumeambiwa kwamba hatusifu ila nimeamua kutoa sifa zifuatazo, kwanza nampongeza Mkuchika kutoa semina ya utawala bora Mkoa wa Iringa, na ninashangaa kuona viongozi wengine wakiendelea kutofuata utaratibu wa Mkuchika, lakini hawa Wakuu wa Mikoa wengine wanapagawa sana wanafika hawamjali mtu yeyote ikiwezekana Waziri Mkuu na TAMISEMI muendelee kuwalea hawa vijana kwa sababu haya mambo ya kuwaweka watu ndani yanashusha ari ya kufanya kazi”, amesema Msigwa.

Hata hivyo, wakati Mbunge Msigwa akisema hayo, Mbunge wa Chemba, Juma Nkamia alibainisha kuwepo kwa tatizo kama hilo wilayani Chemba ambapo zaidi ya watumishi 30 alidai waliomba kuhamishwa kwa sababu viongozi wao kuwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Mfumuko wa bei wa taifa waendelea kushuka hadi asilimia 3.0
CCM hata wakitawala milele mimi sina tatizo- Godbless Lema

Comments

comments